• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu/Majukumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

WILAYA YA MWANGA KUWA NA MTIHANI MMOJA KWA SHULE ZOTE

Posted on: April 10th, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kupitia Idara ya Elimu Sekondari, kuanzia muhula wa kwanza wa mitihani wa mwezi Juni 2018, itakuwa na mtihani mmoja unaofanana kwa Wilaya nzima, kuanzia kidato cha kwanza, hadi kidato cha sita. Utaratibu huu wa kufanya mtihani wa mfanano kwa shule zote za Wilaya, utakuwa endelevu na utafanyika kwa mihula yote kwa kila mwaka.

Akizungumza kwenye kikao kazi na Wakuu wa shule za Sekondari za Serikali na binafsi, Afisa Elimu Sekondari Ndg. Chacha Megewa amesema mtihani huo utajumuisha shule zote za binafsi na za serikali. Amesema kuwa lengo kubwa la kuja na mpango huo ni ili kuinua taaluma ndani ya Wilaya ya Mwanga na kuifanya Wilaya iwe juu zaidi kimkoa na kitaifa. Pamoja na kuwa mtihani huo utachangia kuinua kiwango cha taaluma, pia utakuwa na faida kwa kuleta ushindani kati ya shule na shule, kuimarisha kiwango cha ufaulu, kuimarisha na kuendeleza vipaji, kuwezesha shule kumaliza muhtasari kwa wakati na itasaidia kutatua changamoto za kitaaluma kwa karibu zaidi.

Katika kuhakikisha kuwa mpango huo unakuwa na manufaa, Ndg. Chacha aliunda timu maalum iliyokwenda Jijini Arusha na kujifunza ni kwa namna gani Jiji hilo lilivyoweza kulisimamia jambo hilo na kuweza kuwa la manufaa kwa shule zake kwani, Jiji la Arusha, ndio walioanza mpango huo na umeonekana kuwa, utakuwa na manufaa sana kwa shule za Wilaya ya Mwanga.

Nao Wakuu wa shule wamelipokea jambo hili kwa furaha, na kusema kuwa wapo tayari kulifanyia kazi kwa kuonyesha ushirikiano kwa asilimia mia moja. Wakuu wa shule hao wamesisitiza kuwa maoni yatakayowasilishwa kwao na kamati iliyoteuliwa, ambapo maoni hayo yatakuwa yanaeleza namna ya kuendesha mtihani huo, watakuwa tayari kuyafanyia kazi mawazo ya kamati na watayasimamia ili kuhakikisha mtihani huo unafanyika kama walivyokubaliana.

Samba na hilo, Afisa Elimu Ndg Chacha, alitumia kikao kazi hicho, kuwakumbusha Wakuu wa shule kuhusu namna ya kuendelea kuwa na utendaji kazi bora, kwa kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano. Amewaonya baadhi ya Wakuu wa Shule kuzembea kuleta taarifa za miradi ya ujenzi ofisini kwake. Akiongea kwa msisitizo Ndg Chacha alisema, haiwezekani mradi upo shuleni kwako na taarifa huleti ofisini kwangu, badala yake unasubiri hadi nikuombe taarifa hizo. Amesema taarifa ni vizuri azione kwasababu lengo la taarifa ni kuonyesha uwazi, na hii itaepusha kutiliwa shaka kwenye mradi husika.

Kuhusu suala la maendeleo ya shule, Ndg Chacha amesisitiza, ili shule ziweze kufanya vizuri ni lazima Wakuu wa shule wahakikishe wanafunzi wanapatiwa chakula cha mchana, na amewasisitiza Wakuu wa shule kuhakikisha wanalisimamia vizuri suala hili kwa kuwashirikisha wazazi, Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji na Waratibu Elimu Kata. Ameendelea kusema kuwa, kwa shule ambayo haina bodi, kuanzia sasa bodi ianzishwe kwani haiwezekani shule kuendeshwa bila bodi. Pia amekemea tabia ya baadhi ya walimu kutembea na wanafunzi na hata wakati mwingine kuwapa mimba. Amewaagiza Wakuu hao kuhakikisha wanasimamia nidhamu za walimu na wanafunzi wao ili waweze kuboresha elimu kwenye shule wanazo zisimamia.

Matangazo

  • Tangazo la nafasi za Wajumbe wa Bodi ya Afya ya Halmashauri, Kamati za usimamizi ngazi ya Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kipindi cha kuanzia Julai, 2018 hadi Juni 2021 April 19, 2018
  • Siku ya kupanda miti Kimkoa kufanyikia Wilayani Mwanga Tar 06 Aprili, 2018 April 04, 2018
  • HAFLA YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM TAR 06 MACH, 2018 February 28, 2018
  • SIKU YA WANAWAKE TAREHE 08 MACHI, 2018 March 02, 2018
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • Taasisi ya Elimu ya Green Bird yazidi kuendeleza michezo Mwanga

    April 21, 2018
  • WILAYA YA MWANGA KUWA NA MTIHANI MMOJA KWA SHULE ZOTE

    April 10, 2018
  • Mtoto Anthony mwenye uwezo wa ajabu apata ufadhili

    April 09, 2018
  • TARURA INAVYOCHAPA KAZI WILAYANI MWANGA

    April 05, 2018
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Greenbird college round about to Bomani road

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 2757652

    Namba ya Simu: +255652565207

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa